Mizigo yaanza kuwafikia NATO Afghanistan

Afisaa wa Pakistan kwenye mpaka na Afghanstan, Fazal Bari, anasema lori la kwanza lililobeba mizigo ya vikosi vya Marekani na NATO limevuka mpaka kuingia Afghanistan.

Hata hivyo madereva wengi wa Malori katika bandari ya Karachi wanasema bado hawajapewa ruhusa ya kuvuka mpaka .

Barabara hiyo ya kusafirishia misaada ya vikosi vya NATO na Marekani imefunguliwa baada ya kufungwa kwa miezi saba na maafisa wa Pakistan .

Waliamua kuifungua baada ya kukubali msamaha ulioombwa na Marekani kwa mashambulio ya anga iliyofanya mwezi Novemba yaliyowauwa wapakistan wanne. Barabara hiyo ilifunguliwa rasmi jana baada ya mwezi mzima wa mazungumzo yaliyoilazimisha Marekani kuomba msamaha