Ulinzi uko sawa Olimpiki ya London

Huku ikiwa imesalia wiki mbili kuanza kwa michezo ya olimpiki, serikali ya uingereza imekuwa ikitetea vikali mipango yake ya usalama baada ya kuongeza maelfu ya wanajeshi kulinda maeneo ya michezo hiyo.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Olimpiki mjini London

Waziri wa mambo ya ndani wa uingereza Theresa May aliliambia bunge kuwa usalama katika maeneo ya michezo hiyo umepangwa vilivyo lakini akasema kuwa kumezuka hofu kuhusiana na uwezo wa kampuni ya ulinzi ya G4S kuwafunza wafanyikazi tosha.

Zaidi ya wanajeshi elfu tatu mia tano wameitwa na kufikisha alfu kumi na saba walinzi katika mashindano hayo.