Brotherhood Jordan kususia uchaguzi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mfalme Abdullah wa Jordan

Muslim Brotherhood nchini Jordan imetangaza kuwa watasusia uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanywa mwishoni mwa mwaka.

Msemaji wa Brotherhood amesema baraza lao linalotawala lilipiga kura kususia uchaguzi huo.

Hii ni kutokana na kile walichodai ni kuzorota kwa mageuzi ya kisiasa nchini humo.

Muslim Brotherhood ambacho ndicho chama kikuu cha upinzani nchini Jordan kimesema huenda kikabadili msimamo wake ikiwa Mfalme Abdullah atatoa uhakikisho kuwa mchakato wa mageuzi utaendelea.

Hatua hiyo ya kugomea uchaguzi ni pigo kwa Mfalme huyo wa Jordan aliyeahidi kufanya mageuzi kama njia ya kuzuia maandamano zaidi nchini humo.