ICC yatoa vibali waasi DRC wakamatwe

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita , imetoa vibali vya kukamatwa kwa wababe wawili wa kivita kwa vitendo vya uhalifu wa kivita Mashariki mwa DRC.

Mmoja wa waasi hao ni Sylvestre Muducumura,kiongozi wa kundi la waasi wa FDLR.

Anatuhumiwa kwa makosa tisa ya jinai ikiwemo mauaji , ubakaji na mateso.

Mahakama hiyo pia iliduurusu kibali kingine cha kukamatwa kwa jenerali wa zamani jeshini Bosco Ntaganda, aliyeongoza uasi nchini humo.

Wakati huu Ntaganda anatuhumiwa kwa kuendeleza vita vya kikabila, kuwaweka watu kama wafungwa wa kingono pamoja na ubakaji.