Mahakama ya Thailand kuamua katiba

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Waziri Mkuu wa Thailand Yingluck Shinawatra

Mahakama ya kikatiba nchini Thailand inaratajiwa kutoa uamuzi ambao huenda ukasababisha mgawanyiko mkubwa zaidi wa kisiasa nchini humo.

Majaji wataamua ikiwa wanasiasa wana haki ya kuanza shughuli ya kuandika katiba mpya ya nchi hiyo na ikiwa wale wanaoendesha shughuli hiyo wanahujumu ufalme wa nchi hiyo.

Ikiwa mahakama itatoa aumuzi dhidi ya chama tawala, chama hicho huenda kikavunjwa.

Waandishi wa habari wanasema uamuzi kama huo huenda ukasababisha wafuasi wa chama hicho kufanya maandamano makubwa.