Asasi za kijamii kudhibitiwa Urusi

Bunge la waakilishi nchini Urusi, limepigia kura mswaada ambao utashurustisha mashirika ya kibinadamu nchini humo yanapokea msaada kutoka nje kusajiliwa kama mashirika ya kigeni.

Kwa mujibu wa serikali, ikiwa mswaada huo utaidhinishwa na kuwa sheria, utalinda Urusi kutokana na muingilio wa nchi za kigeni.

Wakosoaji wanatuhumu serikali kwa kujaribu kuzuia upinzani wowote dhidi ya serikali.

Wizara ya mambo ya ndani Marekani, imesema kuwa raia wa urusi kama raia wa nchi yoyote ile, wanahitajika kusikika.

Kwa upande wake, Urusi, imeshutumu Marekani kwa kuingilia sana mambo yake ya ndani.

Yeyeyote anayevunja sheria hiyo huenda akafungwa muda mrefu jela. Miswaada hiyo inatarajiwa kudhnishwa na bunge la Senate kabla ya kutiwa saini na rais Vladimir Putin na kuwa sheria.