Waziri wa Somalia auawa

Waziri wa zamani wa Biashara nchini Somalia Mohamud Ibrahim Garweyne ameuawa katika shambulio la bomu iliyotegwa ndani ya gari mjini Mogadishu.

Polisi wamesema bomu hilo lililipuka nje ya hoteli moja ambayo ni maarufu na wanasiasa wa Somalia.

Katika tukio hilo watu sita walijeruhiwa. Wapiganaji wa kundi la Al Shabaab wamekiri kuhusika na mauaji ya leo.