UNESCO yakosolewa kwa tuzo yake

Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yamesema kuwa ni aibu kubwa na kejeli kwa haki za binadamu kwa hatua ya shirika la Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO, kutoa tuzo ya sayanasi inayofadhiliwa na Rais wa Equatorial Guinea, Teodoro Obiang Nguema Mbasogo.

Mashirika hayo yanamtuhumu Rais huyo kwa uporaji wa mali ya umma na ukiukaji wa haki za binadamu katika nchi ambayo ina viwango vikubwa vya umaskini.