HSBC ilikiuka sheria za benki Marekani

Ripoti ya kamati ya baraza la Senate la Marekani imeishutumu moja ya benki kubwa kuliko zote duniani ya HSBC, kwa kuiweka Marekani katika hatari ya mambo yasiyokubalika kutoka magenge ya wafanyabiashara ya dawa za kulevya na magaidi.

Ripoti hiyo inasema kampuni tanzu ya benki hiyo nchini Marekani ilishindwa kujilinda kutokana na biashara haramu ya fedha.

Kwa mujibu wa wachunguzi, kiasi kikubwa cha fedha kiliingia nchini Marekani kutoka benki ya HSBC tawi la Mexico- zikiwa dola bilioni saba katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili, ikimaanisha kuwa kiasi fulani cha fedha hiyo kilitokana na biashara ya dawa za kulevya.

HSBC imesema itaomba radhi kwa makosa hayo wakati watendaji wake wakuu watakapofika mbele ya kamati ya Senate baadaye leo.