Shambulizi la kombora shuleni Nigeria

Mtoto mwenye umri wa miaka kumi amefariki baada ya kombora kurushwa katika shule moja mjini Jos, Nigeria .

Kwa mujibu wa maafisa wakuu, kombora hilo lilikosa lengo lake na badala yake kugonga jengo moja karibu na shule hiyo.

Maafisa wa shule wanasema kuwa mtoto huyo hakuwa mwanafunzi katika shule hiyo kubwa inayomilikiwa na jamii ya kiisilamu.

Mwandishi wa BBC mjini Jos, Ishaq Khalid anasema kuwa wanafunzi wa shule hiyo walikuwa wanafanya mitihani yao wakati wa shambulizi hilo.

Mji wa Jos uimekuwa kitovu cha mapigano ya kikabila pamoja na mapigano ya kidini katika miaka ya hivi karubini.,

Jos ni mji mkuu wa jimbo la Plateau ambalo liko katika eneo linalogawanya maeneo ya kikristo na yale ya kiisilamu ya Kaskazini.