China yaahidi mabilioni kwa Afrika

Rais wa China Hu Jintao ameziahidi serikali za kiafrika mkopo wa dola bilioni ishirini katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Amesema mkopo huo utasaidia miundo mbinu, kilimo na maendeleo ya biashara. Rais Hu alikuwa akiwahutubia viongozi wa kiafrika katika ufunguzi wa mkutano juu ya ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imeibuka kuwa mshirika mkubwa wa kibiashara na uwekezaji barani Africa wakati ikitafuta mali ghafi kwa ajli ya kuendeleza uchumi wake unaokuwa.