Mapigano zaidi kugombea Walikale Congo

Kuna mapigano mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kugombania kutawala mji wa Walikale.

Waasi wa vuguvugu la Mai Mai walishambulia sehemu za jeshi la Congo siku ya Jumanne. Timu kutoka shirika la kitabibu la kujitolea MSF, wanasema wanashindwa kuondoka eneo lao kwenda kusaidia kundi kubwa la watu wapatao elfu ishirini.

MSF inasema iwapo hali itazidi kuendelea kuwa mbaya zaidi, wafanyakazi wao wa afya itabidi waondolewe huko.

Walikale eneo lililoko magharibi mwa jiji la Goma, ni kiini cha eneo tajiri la madini, ambalo limekuwa likipiganiwa kwa miezi kadhaa.