Mohamed Bin Hammam wa FIFA hana hatia

Mahakama ya sheria katika michezo imetengua adhabu ya rushwa FIFA iliyotoa kwa Mohamed Bin Hammam aliyegombea kiti cha rais wa FIFA mwaka jana.

FIFA ilimzuia katika michezo kwa madai ya kuhusika na rushwa kwa maafisa wa FIFA wakati wa kampeni za uchaguzi wa urais dhidi Sepp Blatter, rais wa FIFA.

Mahakama hiyo imesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kesi dhidi ya bwana Bin Hammam. Hata hivyo shirikisho la soka la bara Asia, bado linashikilia msimamo wake wa kumsimamisha kuhusiana na mapungufu katika chama hicho kama rais wao.