Kiongozi wa zamani wa Chad kushtakiwa

Mahakama ya kimataifa imetoa uamuzi kuwa nchi ya Senegal lazima ianze utaratibu wa kumfungulia mashitaka kiongozi wa zamani wa Chad, Hissene Habre bila kuchelewa.

La sivyo apelekwe nchini Ubelgiji kufunguliwa mashitaka, hukumu hiyo yenye nguvu kisheria imesema.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 69 amekuwa akishikiliwa katika nyumba nchini Senegal toka mwaka 2005 alipokimbilia baada ya kuondolewa madarakani nchini Chad.

Kiongozi huyo anakanusha mashitaka ya mauaji na kuwatesa maelfu ya wapinzani wake.

Makosa hayo yanahusishwa kuanzia mwaka 1982, wakati Bwana Habre alipoingia madarakani, hadi alipotimuliwa mwaka 1990.