Rufaa ya Ai Weiwei yakataliwa

Mahakama moja nchini China imekataa rufaa iliyowasilishwa na mpinzani wa serikali nchini humo Ai Weiwei kupinga adhabu ya zaidi ya dola milioni mbili kwa kosa la kukwepa kulipa kodi.

Mpinzani huyo wa serikali ambaye ni msanii alizuiwa kuhudhuria uamuzi huo wa mahakama iliyokuwa na ulinzi mkali mjini Beijing.

Amesema hukumu hiyo imethibitishia dunia kuwa utawala wa sheria na haki haupo nchini China.

Wafuasi wa Ai Weiwei daima wanachukulia kesi hiyo ya kukwepa kodi kama jaribio la serikali hiyo ya Kikomunisti kumnyamazisha mpinzani wake huyo.