Afisa mwingine wa Assad afa nchini Syria

Huku mapigano mjini Damascus na kwengineko yakipelekea maelfu kukimbilia lebanon kwa usalama wao, serikali imetangaza kuwa afisa mwengine wa ngazi za juu amefariki kutokana na majeraha aliyopata.

Marehemu Hisham Ikhtyar mkuu wa idara ya ujasusi alijeruhiwa kwa bomu katika makao makuu ya usalama mjini humo hapo siku ya jumatano.

Hadi sasa yeye ni afisa wa nne wa ngazi za juu kuuwawa wiki hii.

Kituo cha habari za serikali kinasema serikali imechukua udhibiti wa wilaya, kusini mwa Damascus iliyokuwa imetwaliwa na waasi.