Mangariba wahukumiwa jela Senegal

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini Ivory Coast, wamepongeza hukumu ya kifungo jela iliyotolewa kwa mangariba tisa au wanawake wanaopasha tohara kwa kitendo cha kuwapasha tohara wasichana wadogo.

Kitendo hicho kimeharamishwa nchini Ivory Coast kwa miaka kumi na minne sasa.

Lakini ni mara ya kwanza kwa mtu yeyote kuhukumiwa kwa kitendo cha upashaji tohara.

Mwanaharakati mashuhuri wa kutetea haki za wanawake, Constance Yai, ammesema uamuzi huo huenda ukawapa motisha majaji wengine kutoa hukumu sawa na hiyo kuhusiana na visa vya upashaji tohara.

Utafiti uliofanywa ulionyesha kuwa zaidi ya thuluthi moja ya wanawake wote nchini Ivory Coast wamepashwa tohara licha ya miradi mingi tu ya kuhamasisha watu dhidi ya upashaji tohara.