Madawa ya HIV yafurahisha wanasayansi

Haki miliki ya picha na
Image caption Madawa ya kupunguza makali ya Ukimwi

Wanasayansi wametangaza matokeo ya awali kuwa mseto mpya wa dawa tatu umeonyesha ufanisi katika kutibu ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa ambao unaua watu milioni moja na nusu kwa mwaka duniani, ukiongoza kwa kusababisha vifo pamoja na Ukimwi.

Matokeo ya majaribio ya kwanza yameonyesha kuwa mchanganyiko wa dawa hiyo unafanyakazi kwa ufanisi zaidi ikilinganishwa na dawa zinazotumika sasa.

Watafiti wanasema majaribio ya wiki mbili yaliyofanyika Afrika Kusini yameonyesha kuwa mchanganyiko wa dawa hiyo mpya ilionyesha ufanisi kwa asilimia 99 katika kuua vijidudu vya TB.

Ufuatiliaji wa dawa hiyo kwa kipindi kirefu umeanza.