Mapigano zaidi nje ya Goma

Mapigano makali yameendelea viungani mwa mji wa Goma Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mwandishi wa BBC mjini humo amesema ndege za majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa zimelenga waasi wa M23 ambao Umoja wa Mataifa unatuhumu Rwanda kwa kuwafadhili.

Rubaa zinasema makombora ya majeshi ya Umoja wa Mataifa yanasaidia wanajeshi wa Congo kukabiliana na waasi.

Maelfu ya raia wamekimbia mapigano ya sasa ambapo wanapiga kambi mjini Goma na kambi za majeshi ya Umoja wa Mataifa.