Kim Jong-un amepata jiko

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un sio kapera tena.

Taarifa za runinga ya kitaifa imesema kiongozi huyo ameshiriki tamasha la ufunguzi wa bustani ya maonyesho akiandamana na mkewe aliyetajwa kama ,Ri Sol-ju,.

Mwana mama huyo amekua akionekana na Kim Jong-un katika mikutano rasmi japo vyombo vya habari havikutoa taarifa zake.