majeshi ya Syria yaelekea Aleppo

Image caption Majeshi ya upinzani mjini Aleppo

Idadi kubwa ya wanajeshi ya Syria wameripotiwa kuelekea katika mji wa Aleppo wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Hii inaonekana kama sehemu ya jitihada ya kuyatwaa maeneo ya mji huo ambayo kwa sasa yanashikiliwa na waasi.

Wapiganaji wa upinzani wa Free Syrian Army wamesema maelfu ya askari wakiwa na vifaru na magari ya deraya walmekuwa wakiondoka jimbo la Idlib karibu na mpaka wa Uturuki ili kuelekea Aleppo.

Vikundi vya upinzani vinasema maeneo ya vitongoji vya mji wa Aleppo na mji mkuu Damascus yameshambuliwa kwa silaha nzito wakati serikali ikijaribu kurejesha udhibiti wake katika maeneo hayo.