Maiti zaidi zatolewa baharini, Zanzibar

Maiti zaidi zinaendelea kutolewa baharini kufuatia ajali ya boti kisiwani Zanzibar.

Boti hio ilizama wiki jana na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100.

Wamiliki wa boti hio akiwemo nahodha na maneja wa kampuni ua meli hio kwa jina MV Skagi wameshtakiwa kwa mauaji bila kusudia.

Mwaka jana boti nyingine ilizama kisiwani Zanzibar na kusababisha vifo vya watu wengi.

Meli zinazoendesha huduma zake kisiwani humo zimekua zikiwabeba abiria kupita kiasi kinachokubalika.