Mwenge wa Olimpik washangiliwa Uingereza

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwenge wa Olimpiki wapokewa kwa shangwe

Mwenge wa olimpiki umepitia katika maeneo ya kihistoria mjini london ikiwemo kanisa kuu la St Paul, ukumbi wa sanaa wa Tate Modern art gallery na ule wa Shakespeare's Globe theatre katika siku ya mwisho ya mzunguko wake.

Utaelekea katika barabara ya Downing Street kabla ya kupitia katika makao ya kifalme ya Buckingham mbele ya Prince William na mkewe.

Kilele cha mzunguko huo hii leo kitakuwa tamasha katika bustani ya Hyde Park kabla ya kupelekwa katika ukumbi wa olimpiki tayari kwa hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo hiyo kesho ijumaa.