Free Syrian Army wadhibiti Aleppo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mapigano makali aleppo

Mwandishi mmoja wa habari aliye katika mji mkuu wa pili nchini Syria, Aleppo, ameiambia BBC kuwa waasi kutoka kwa kundi la Free Syrian Army wanaonekana kudhibiti nusu ya mji huo.

Hata hivyo, mwandishi huyo kutoka Ufaransa, amesema kuwa waasi hao wanatarajia maelfu ya wanajeshi wa serikali ndani ya vifaru kujaribu kuwa'ngoa.

Mwandishi huyo amesema waasi hao wanapanga kuvamia na kuviharibu vifaru hivyo vya serikali.

Ameongezea kuwa aliona helikopta na ndege za kivita za serikali zikipaa katika anga za Aleppo hapo jana, huku waasi wakizishambulia kwa risasi.