Wahamiaji wasomali 90 wakwama baharini

Boti moja iliyo na wahamiaji tisini kutoka somalia imekwama katika ziwa Mediterranean.

Mmoja wa wahamiaji hao aliipigia simu idhaa ya kisomali ya BBC akisema kuwa mtambo wa boti hiyo umeharibika na kwamba hawana maji ya kunywa.

anasema wahamiaji hao walitoka katika mji mkuu wa libya tripoli siku nne zilizopita wakitumai kufika katika pwani ya italia.

Mamia ya wasomali hujaribu kuvuka eneo hilo kuelekea bara uropa kutafuta maisha bora.