Bolt aonya wapinzani,asema yuko imara

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Usain Bolt

Mtu mwenye kasi zaidi duniani - Usain Bolt wa Jamaica - amekiri kuwa amekuwa na matatizo ya mgongo katika miezi ya hivi karibuni, lakini akaongeza kuwa - kwa sasa ana nafuu ya asilimia tisini na tano, na yuko tayari kushindana.

katika mahojiano na BBC mwanaraidha huyo amewaonya wapinzani wake.

Amesema kuwa michezo ya mwaka huu ya Olimpiki itasaidia kupeana ishara ya jinsi maisha yake ya baadae yatakavyokuwa.