India kuchunguza treni kushika moto

Waziri wa Reli nchini India ametoa amri kufanyike uchunguzi wa moto kwenye treni ya biria ambao umeua watu 32 katika jimbo la Andhra Pradesh.

Treni ya Tamil Nadu Express kutoka Delhi kuelekea Chennai ilishika moto wakati ikielekea kituo cha Nellore mapema Jumatatu.

Chanzo cha moto huo hakijajulikana lakini mamlaka zinasema wanahisi kulikuwa na hitilafu za umeme.The cause of the blaze is still unclear, but authorities suspect an electrical short circuit.

Waziri wa usafiri wa Reli Mukul Roy alisema njama haziwezi kutupiliwa mbali.

Aliviambia vyombo vya habari kuwa msiamizi wa reli kwenye kituo cha Nellore alisikia "sauti kubwa wakati moto ilipotokea kwenye treni hiyo".

"Hakuna kitu ambacho kinaweza kuachwa na hakuna ambacho hakitachungzwa," alinukuliwa akisema kupitia vyombo vya habari.