Zuma ampongeza Sipho kumaliza masomo

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amempongeza mwanamuziki maarufu Sipho "Hotstix" Mabuse kwa kumaliza masomo yake ya sekondari katika umri wa miaka sitini

Mabuse alijiandikisha katika madarasa ya watu wazima karibu na nyumbani kwake Soweto, Johannesburg, baada ya kuacha shule miaka ya 1960.

"Nilitaka kumaliza hesabu zangu za matrix kukamishwa ingawa nimefanikiwa sana kwenye muziki. Miaka 45 nje ya darasa si mchezo wa kitoto, " aliandika kwenye Twitter.

Watu wazima 12% Afrika Kusini hawajui kusoma na kuandika kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.

Tunavutiwa na ujasiri wako, nidhamu na wivu wa kutaka kufanikiwaā€¯alisema Rais Zuma.