Aliyekuwa bosi benki Nigeria kutoa fidia

Benki ya Nigeria ya Access imeshinda kesi mahakama kuu ya London na kuamuru mkuu wa zamani kuilipa benki £600 milioni.

Erastus Akingbola, Mkurugenzi mtendaji wa zamani wa Benki ya Intercontinental aliyeajiriwa na benki ya Access mwaka uliopita, ameamuriwa kulipa fedha hzio baada ya kukutwa ba hatia ya kujipatia hisa isivyo halali.

Intercontinental waliwekewa dhamana na Benki kuu ya Nigeria mwaka 2009

Jaji aliamua kuwa Bw mipango ya Akingbola ilichangia kufilisika kwa benki. Bw Akingbola alikanusha kufanya makosa yoyote.

Kesi hiyo ilisikilizwa mjini London kwa sababu mshtakiwa alikuwa akiishi mjini humo wakati kesi ikisikilizwa.