Video ya waasi wakiua yawekwa mtandaoni

Picha ya video iliyochapishwa kwenye mtandao inaonyesha waasi katika mji wa Aleppo wakiwaua wanaume wanaowatuhumu kuwa ni miongoni mwa wapiganaji wanaomuunga mkono Rais Bashar Al Assad.

Waasi hao wanasema wote waliouawa ni kutoka ukoo unaogopeka wa wapiganaji wa Shabiha ambao wamekuwa wakiendesha mauaji katika mji huo.

Afisa mwandamizi wa jeshi la upinzani amesema kitendo hicho ni sawa na waasi kupigana wenyewe dhidi ya utawala jeuri.

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch limealaani mauaji hayo.