Kampuni ya Telkom Afrika Kusini yafainiwa

Kampuni rasmi ya mawasiliano ya simu nchini Afrika Kusini, Telekom, imetozwa faini ya dola milioni hamsini kwa kuwadhulumu washindani wake kwa kutumia ukiritimba wake visivyo.

Wadhibiti wa serikali waligundua kuwa kampuni hiyo ilizitoza pesa nyingi sana kampuni washindani wake kwa huduma zake za internet.

Wadhibiti wanasema hatua hii ya Telkom, imeathiri ubunifu na vile vile kuwaatahiri wateja.

Serikali ya Afrika Kusini ndiyo inamiliki aslimia kubwa ya hisa katika shirika la Telekom, ambalo ndio la pili kwa ukubwa katika utoaji wa huduma za simu.