Afrika Kusini kusimamia mpango wa HIV

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton, anatarajiwa kutia saini makubaliano ambayo yatapelekea Afrika Kusini kuongoza mpango wa Marekani wa kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi Afrika.

Dola bilioni tatu nukta mbili tayari zimetukika kwenye mpango huo hasa kugharamia madawa ya kupambana na makali ya virusi vya HIV, matibau na kampeini ya kuhamasisha nyenzo za kupambana na maambukizi mapya.

Mpango huo ulianzishwa mwaka 2004.

Afrika Kusini ndio nchi yenye idadi kubwa ya maambukizi ya HIV kote duniani ikiwa natakriban watu milioni tano nukta nane walioambukizwa virusi hivyo.

Hii inakisiwa kuwa asilimia kumi na nane ya idadi ya watu chini humo.