Akiri kosa la mauaji ya Anni Dewani

Mahakama moja nchini Afrika Kusini imempata na hatia mwanaume mmoja kwa mauaji ya mwanamke raia wa Sweden, Anni Dewani wakati wa fungate yake na mumewe mjini Cape Town mwaka 2010 .

Mziwamadoda Qwabe amehukumiwa miaka 25 gerezani.

Mziwamadoda alishtakiwa pamoja na mumewe marehemu Shrien Dewani raia wa Uingereza na mshukiwa mwingine raia wa Afrika Kusini Xolile Mngeni.

Dewani ambaye ni mumewe marehemu , amekana kupanga njama ya kumuua mkewe na ameenda mahakamani kuzuia arudishwe nchini Afrika Kusini ili ili kujibu kesi dhidi yake.

Mshukiwa mwenzake, Mngeni ana uvimbe kwenye ubongo wake hali ambayo hadi kufikia sasa imemzuia kufunguliwa mashtaka.

Wakili wa utetezi Daniel Theunissen, aliambia mahakama kuu kuwa Qwabe alikubali kukiri kosa la utejkaji nyara, wizi , mauaji na kumili silaha kinyume na sheria