Iran yakana sio mahujaji tena

Iran imekiri kwa mara ya kwanza kuwa kundi la mateka arobaini na wanane wanaozuiliwa nchini Syria linajumuisha waliokuwa wanajeshi wa Iran.

Tehran ilikuwa imesisitiza kuwa kundi hilo lilijumuisha mahujaji waliokuwa ziarani nchini Syria.

Waasi wa Syria wanaowashikilia wanasisitiza kuwa watu hao wanatumiwa na jeshi la Syria kufanya ujasusi.

Iran imetoa wito kwa Umoja wa mataifa kusaidia kuwakomboa mateka hao.