Mazishi ya hayati John Atta Mills

Hafla ya mazishi ya siku tatu inaanza leo nchini ghana ya kumpa heshima za mwisho aliyekuwa rais wa nchi hiyo John Atta Mills aliyefariki wiki mbili zilizopita.

Mwili wake unatarajiwa kulazwa katika ukumbi maalum karibu na jengo la bunge hadi atakapozikwa silu ya Ijumaa.

Viongozi wengi wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria maziko hayo akiwemo waziri wa masuala ya nje wa Marekani Hallary Clinton.

Bwana Mills alikuwa mwanazuoni mkuu aliyeingia uongozini mwaka wa elfu mbili na tisa na kuhudumu kama rais hadi kifo chake.