Wakenya kumi wafa ajalini Tanzania

Takriban raia kumi wa Kenya wanahofiwa kufa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupata ajali nchini Tanzania.

Basi hilo lililoanguka katika eneo la Tanga, kaskazini mwa Tanzania, lilikuwa limebeba wanawake sitini raia wa Kenya waliokuwa katika ziara ya kanisa nchini humo.

Ripoti zinasema kuwa watu sabini na watano wamejeruhiwa kutokana na ajali hiyo na wengi wamepelekwa katika hospitali ya Tumbi.