Gbagbo sasa kusomewa mashtaka rasmi

Aliyekuwa rais wa Ivory Coast aliyeondolewa madarakani kwa lazima Laurent Gbagbo atafikishwa kizimbani katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita ya ICC mjini The Hague siku ya Jumatatu, kusomewa rasmi mashtaka yanayomkabili.

Bwana Bgabo anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita kufuatia mapigano yaliyoikumba Ivory Coast baada ya uchaguzi wa urais uliopita.