Marufuku kubeba silaha za asili India

Imebadilishwa: 14 Agosti, 2012 - Saa 19:23 GMT

Serikali katika jimbo la katikati mwa India la Chhattisgarh imepiga marufuku watu wa makabila kubeba silaha za kiasili katika maeneo ya wazi.

Silaha hizo zinajumuisha upinde na mishale, mundu na shoka.

Maafisa wa polisi wamesema hatua hiyo inafuatia kuongezeka kwa mashabulizi kutoka kwa kundi la waasi la Maoist.

Hata hivyo hatua hiyo imekosolewa na baadhi ya makabila wanaosema kuwa inakiuka haki za watu wa makabila hayo.

Waasi wa Maoist nchini India wamekuwa wakifanya shughuli zao katika majimbo mbalimbali nchini India lakini jimbo la Chhattisgarh ni moja kati ya yanayoathiriwa zaidi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.