Vigogo wazozana Somalia kampeni ikianza

Imebadilishwa: 16 Agosti, 2012 - Saa 03:31 GMT

Katika hali inayohofiwa kuathiri mchakato wa kuunda serikali mpya nchini Somalia, viongozi wa juu wa nchi hiyo wamerushiana maneno makali kupitia vyombo vya habari.

Rais Sharif Sheikh Ahmed amemshutumu vikali Waziri Mkuu wake Abdiweli Mohamed Ali kwa kuingilia mamlaka ya rais, wakati Waziri Mkuu akimshutumu rais kwa kukiuka katiba ya nchi.

Viongozi hao wawili wote ni wagombea katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Hali ya wasiwasi imewakumba viongozi wengi wa Somalia wanaongangania kushinda Urais katika uchaguzi utakaofanywa na Wabunge wanaoendelea kuteuliwa kutoka koo mbalimbali kote nchini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.