Waandamaji wauawa Afrika Kusini

Imebadilishwa: 17 Agosti, 2012 - Saa 04:22 GMT

Polisi nchini Afrika Kusini wamewaua wachimba migodi kadhaa na kuwajeruhi wengine wengi katika juhudi za kuwatawanya waandamanaji waliokuwa wakilalamikia mishahara duni.

Mwandishi mmoja aliyekuwepo nje ya mgodi wa Lonmin Platinum wa Marikana aliambia BBC kuwa polisi walionekana kushambulia mfano wa siku za ubaguzi wa rangi.

Waliojeruhiwa walisafirishwa kwa helikopta hadi hospitalini.

Waandamanaji hao, wachimba migodi, walikuwa wakidai nyongeza ya mshahara wa Dola 1,500 kwa mwezi.

Polisi walisema mashauriano kati ya wawakilishi wa wafanyakazi wa Association of Mine Workers and Construction (AMCU) yalikwama na ikalizimika kuwatimua wafanyakazi hao kutoka mahali pale kwa nguvu.

Polisi walikuwa wakifanya maamuzi wakati ambapo wachimba migodi walikuwa wameshika mikononi silaha za kitamaduni na bunduki.

Rais Zuma amenukuliwa akisema kuwa amesikitishwa sana na mauaji hayo yasiyokuwa na maana. Chama cha upinzani cha upinzani cha Democratic Alliance limetoa wito Serikali kuunda tume ya kuchunguza kilichosababisha mauaji hayo.

Ghasia zilianza mapema juma hili baada ya makundi mawili ya kuwakilisha wachimba migodi kupigana na kusababisha vifo vya watu kumi, kukiwemo maafisa wawilai wa polisi.

Afrka Kusini ni taifa linalozalisha madini aina ya Platinum kwa wingi zaidi duniani.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.