Uingereza, Ecuador Wazozania Assange

Imebadilishwa: 17 Agosti, 2012 - Saa 05:06 GMT

Uamuzi wa Ecuador kumpa hifadhi ya kisiasa mwanzilishi wa mtandao wa wikiliks, Julian Assange, ambaye anaendelea kujificha kutoka kwa maafisa wa polisi wa Uingereza kwa mwezi wa pili katika ubalozi wa Taifa hilo, umezua sintofahamu kubwa kati ya Uingereza, Ecuador na Sweden.

Assange anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na ubakaji wa wanawake kadhaa nchini Sweden na Mahakama ya Uingereza iliamuru kuwa akamatwe na kusafirisha hadi Sweden kukabiliana na mashtaka yanayomkabili.

Mara tu baada ya Serikali ya Ecuador kutanganza kuwa imempa hifadhi ya kisiasa Bwana Assange, Serikali ya Uingereza ilitisha kutumia sheria ya mwaka wa 1987 kumtoa kwa nguvu Assange kutoka ubalozi wa Ecuador mjini London.

Chini ya sheria hiyo Wakati huohuo Serikali ya Sweden nayo ilitoa taarifa ya kushutumu Ecuador ikisema kuwa hatua hiyo ya Ecuador ni juhudi za taifa hilo kuvuruga mpango wa kisheria wa Sweden na kuvuruga ushirikiano wa kisheria kati ya mataifa ya Ulaya.

Madai ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ecuador kuwa Utaratibu wote wa kisheria wa Sweden umekumbwa na msukumo wa kisiasa ulimwudhi sana Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Sweden, Carl Bildt, alitangaza kwenye mtandao wa internet kuwa sheria za Sweden ni baadhi ya sheria zilizo kamilifu zaidi duniani.

Hata hivyo kufikia sasa watu wengi wanajiuliza kuwa Bwana Assange atafanya nini sasa kwa sababu hata ingawa ana hifadhi ya kisiasa ya Ecuador, lakini yuko nchini Uingereza, taifa ambalo limeapa kuwa hawatamruhusu aende ko kote. Wamesema huenda wakaingia kwenye ubalozi na kumchomoa.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.