Assange ajitokeza hadharani Uingereza

Imebadilishwa: 19 Agosti, 2012 - Saa 18:56 GMT

Mwanzilishi wa Wikileaks Julian Assange amejitokeza hadharani kwa mara ya kwanza tokea miezi miwili iliyopita.

Alizungumza katika baraza ndogo katika jengo la Ubalozi wa Equador jijini London alipokuwa amepatiwa hifadhi kuepuka kupelekwa nchini Sweden kukabiliana na tuhuma za ubakaji.

Bwana Assange aliushukuru ubalozi wa Ecuador kwa kumpatia hadhi ya ukimbizi na kuikosoa vikali Marekani.

Amesema Washington ni lazima iahidi kutomshitaki kwa kufichua nyaraka za siri na kuacha kile alichokiita kuisakama Wikileaks.

Pia amezilaumu nchi za Uingereza, Sweden na Australia anakotoka kwa kushindwa kumuunga mkono

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.