Atoroka china baada ya tuhuma za ubadhirifu

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 14:18 GMT

Taarifa za vyombo vya habari nchini China zinasema kuwa afisaa mmoja mkuu wa zamani wa chama cha kikomunisti ametoroka baada ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa zaidi ya dola milioni thelathini.

Gazeti linalomilikiwa na chama hicho People Daily, limesema kuwa afisaa huyo, Wang Guoqiang, aliachishwa majukumu yake kabla ya kutoroka nchi hiyo.

Anatuhumiwa kwa kula rushwa na kuekeza katika biashara zake binafsi.

Waziri mkuu Wen Jiabao amekuwa akitoa onyo za mara kwa mara kwamba ufisadi ndio changamoto kubwa kwa chama tawala.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.