Waziri wa zamani ana hatia ya mauaji

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 10:44 GMT

Mahakama moja nchini India imempata na hatia waziri wa serikali kwa kuhusika na mauaji ya halaiki ya waisilamu tisini na tano wakati wa ghasia za kidini katika jimbo la Gujarat miaka kumi iliyopita.

Maya Kodnani aliyekuwa waziri wa mambo ya wanawake, alituhumiwa kwa kuchochea ghasia dhidi ya jamii za waisilamu katika wilaya ya Naroda Patiya mjini Ahmedabad.

Alipatikana na hatia akiwa na mshtakiwa mwenzake ambaye ni kiongozi wa wapiganaji wa kihindu Babu Bajrangi pamoja na washukiwa wengine thelathini.

Ghasia za Gujarat zilizuka baada ya mahujaji sitini wa kihindu kufariki katika ajali ya Treni.

Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa waisilamu waliuawa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.