Wanajeshi 6 wauawa Pakistan

Imebadilishwa: 29 Agosti, 2012 - Saa 10:56 GMT

Maafisa wakuu nchini Pakistan, wamesema kuwa wapiganaji wa Taliban wameshambulia kambi ya jeshi katika eneo la kikabila la Waziristan Kusini na kuwaua wanajeshi sita.

Msemaji wa kundi hilo, ameelezea kuwa wanajeshi kumi na wawili waliuawa katika shambulizi hilo baadhi yao wakikatwa katwa vichwa.

Kwa mujibu wa duru za maafisa wa usalama, wanamgambo tisa waliuawa baadaye katika makabiliano kati ya pande hizo mbili.

Duru zinasema kuwa taarifa zinazotofautiana kuhusu tukio lenyewe ni ngumu kuthibitisha, kwani hakuna njia binafsi ya kuweza kufikia eneo hilo la vijijini.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.