Angola yajiandaa kwa uchaguzi

Imebadilishwa: 30 Agosti, 2012 - Saa 14:18 GMT

Siku moja kabla ya uchaguzi mkuu nchini Angola, chama kikuu cha upinzani nchini humo, UNITA, kimesema hakuna mazingira ya kuwezesha kuwepo kwa uchaguzi ulio huru na wa haki.

Kiongozi wa UNITA, Isaias Samakuva, amesema ameitisha mkutano na Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, kujadili baadhi ya matatizo, ikiwemo suala la kukosa kuweka majina ya wapiga kura wote katika sajili ya wapiga kura.

Kundi la wanaharakati pia limeitisha kucheleshwa kwa uchaguzi huo. Tume ya uchaguzi ya Angola imekanusha kuwepo kwa matatizo au dosara yoyote kwenye sajili ya wapiga kura.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.