Wahamiaji haramu waokolewa Indonesia

Imebadilishwa: 30 Agosti, 2012 - Saa 15:30 GMT


Zaidi ya manusura hamsini wameokolewa nchini Indonesia kutoka kwa boti iliyokuwa imejaa wahamiaji haramu ambayo ilizama katika eneo hilo siku ya Jumatano.

Awali maafisa wa utawala walisitisha shughuli za uokozi baada ya manusura kutopatikana.

Lakini meli moja ya mizigo ya Australia iliweza kuokoa kundi moja la watu kutoka kusini magharibi mwa pwani ya Java.

Takriban wahamiaji haramu miamoja hamsini kutoka nchi kadhaa za bara Asia,walikisiwa kuwa ndani ya boti hiyo iliyokuwa inaelekea nchini Australia.

Shughuli za uokozi zimeweza kusitishwa sasa hadi hapo kesho matumaini ya kupata manusura zaidi yakiwepo.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.