Afisaa wa chama hatiani nchini India

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 15:27 GMT

Mahakama moja nchini India imemhukumu mwanachama wa ngazi ya juu wa chama kinachoegemea mrengo wa kulia cha BJP miaka 28 jela.

Maya Kodnani, alipatikana na hatia ya kosa la kuhusika katika ghasia zilizotokea katika jimbo la Gujarat miaka kumi iliyopita.

Hukumu hiyo dhidi yake ilitolewa siku ya Jumatano baada ya kupatikana na hatia ya mauaji pamoja na jaribio la mauaji.

Washukiwa wengine thelathini na moja pia walihukumiwa.

Wakati wa ghasia hizo, Bi Kodnani alikuwa mwanasiasa katika jimbo hilo ingawa baadaye aliteuliwa kuwa waziri.

Yeye ndiye afisaa wa ngazi ya juu zaidi wa chama kinachotawala jimbo kupatikana na hatia.

Zaidi ya watu elfu moja wengi wao wakiwa waisilamu walifariki katika ghasia hizo zilizotokea katika jimbo la Gujarat .

Ghasia zilizuka siku moja baada ya mahujaji sitini wa kihindu kufariki katika ajali ya moto kwenye treni.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.