Migogoro ya makundi ya Mafia Italia

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 16:36 GMT


Serikali ya Italia inatarajiwa kutuma kikosi cha polisi katika wilaya ya Naples kutokana na kusambaa kwa mapigano kati ya makundi mawili ya kimafia .

Makundi hayo ya mafia yanayojulikana kama 'Camorra' yanazozana kuhusu udhibiti wa mitaa ambayo imetajwa kama maeneo maarufu zaidi barani Ulaya kunakofanyika biashara haramu za mihadarati.

Inakisiwa kuwa biashara hizo ni za thamani ya zaidi ya dola milioni miamoja kila mwaka.

Katika miezi ya hivi karibuni watu 24 wameuwawa kutokana na uhasama baina ya makundi hayo mawili ya kimafia.

Kisa cha hivi karibuni ni kile cha kiongozi mmoja wa kundi moja maarufu la mafia kupigwa risasi wakati akirudi kutoka mapumziko visiwani pamoja na familia yake.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.