Tetemeko kubwa la ardhi Ufilipino

Imebadilishwa: 31 Agosti, 2012 - Saa 15:47 GMT

Tetemeko kubwa la ardhi limeripotiwa kutokea Mashariki mwa Ufilipino na kusababisha baadhi ya wakaazi kukimbilia usalama wao.

Kulikuwa na ripoti za awali zikielezea kutokea uharibifu katika baadhi ya maeneo .

Tahadhari ya kutokea tsunami ilikuwa imetolewa nchini Japan, Taiwan na maeneo mengine ya bahari ya Pacific ingawa baadaye onyo hilo lilifutiliwa mbali.

Tetemeko hilo, lilikuwa la kiwango cha saba nukta sita na lilitokea umbali wa kilomita miamoja na hamsini kutoka kati kati mwa kisiwa cha Samar nchini Ufilipino.

Mkaazi mmoja wa pwani ya Pacific alisema kuwa tetemeko hilo lilisikika kwa muda mrefu na lilikuwa nzito sana ingawa mawimbi yalijongea hadi kwenye ufuo na yaliripotiwa kuwa makali ikilinganishwa na mawimbi ya kawaida.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.